Sekta ya utalii Nchini, imeendelea kunufaika na Filamu ya Royal tour ambayo imefanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongezeka kwa idadi ya wageni wanaokuja kutalii maeneo mbalimbali ya Nchi.

Kauli hiyo imeolewa na Meneja Masoko wa Kili Medair, Peter Sarakikya wakati akizungumza na Dar24 Media katika maonyesho ya Utalii yanayofanyika katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, na kuongeza kuwa pia imetangaza utalii kwa kiasi kikubwa na kuleta ongezeko la wageni Nchini.

 Meneja Masoko wa Kili Medair, Peter Sarakikya.

Amesema, “Wageni kutoka Nchi mbalimbali na hata zile nchi ambazo Wageni walikuwa hawaji kwa namna kubwa Nchini lakini kwasasa wanakuja kwa wingi, na hii yote ni kupitia filamu bora ya Royal tour.”

Akizungumzia Kili Medair, Sarakikya amesema ipo kwa ajili ya kuhakikisha watalii wanakuwa katika hali ya salama pale wanapokuwa katika mazingira ambayo sio salama pindi ambapo wanapata changamoto mbalimbali na wao kutoa usaidizi.

MAKALA: Mbinu za mabosi, rushwa ya ngono
DMI: Vijana changamkieni fursa za Ubaharia