Boniface Gideon – Tanga.

Wakala wa Biashara na Leseni – BRELA, wameendesha zoezi la kutoa Elimu ya alama Miliki Ubunifu Bunifu kwa Wateja na Wadau mbalimbali wanaotembelea mabanda yao kwenye maonesho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika katika Viwanja vya Popatilal, Jijini Tanga.

Akitoa Elimu kwa Wadau na Wamiliki wa Biashara, Msaidizi wa Usajiri Mwandamizi kutoka kurugenzi ya Miliki Ubunifu, Nassoro Mtavu amesema ni vyema kila mtu akapata Elimu ya Mlipakodi ili aweze kusajiri Biashara na Leseni ,

“Kazi kubwa ya maonyesho haya ni kutoa Elimu ya ufumbuzi na alama za Biashara na huduma,kwetu sisi tumeichukulia hii kama fursa ya kutoa Elimu,na tukumbuke kuwa sehemu ya Elimu hii ni uvumbuzi,na sisi Brela uvumbuzi ndio kazi kubwa tunayoifanya ,wengi hawafahamu nini Cha kufanya baada ya kuvumbua kitu , kwahiyo tunachokifanya nikuwapatia Elimu sahihi nini chakufanya baada ya kuvumbua,” amesisitiza Nassoro.

Msaidizi wa Usajiri Mwandamizi kutoka kurugenzi ya Miliki Ubunifu, Nassoro Mtavu.

Amesema, wataendelea kutoa Elimu juu Usajiri wa Biashara na Leseni nakuwataka wadau mbalimbali kuhakikisha wanasajiri huduma mbalimbali wanazozitoa akiongeza kuwa, “tunawaomba Wadau wetu wasajiri huduma wanazozitoa ili ziwe na vibali ,na sisi tupo tayari wakati wowote kutoa huduma,na tutaendelea kushirikiana na Wadau wetu na wasichoke kutuuliza pale wanaposhindwa kutimiza vigezo.”

Amesema kwasasa kusajiri Biashara na kupata Leseni za ‘BRELA’ ni rahisi na wanaweza kupata huduma kwanjia ya mtandao, “”unaweza kupata huduma kwanjia ya mtandao na ukapata huduma ,pia tunawaomba wavumbuzi waje kwetu ,waache kusikiliza maneno ya mtaani mana watapotoshwa na watapata Elimu isiyo sahihi,” alimesema Nassoro.

Wazalishaji Vyakula vya Mifugo waonywa, sheria kuwakabili
Mtuhumiwa wa mauaji, msafirishaji dawa za kulevya wanaswa Arusha