Shirika la Umeme Nchini, limewahimizap Wananchi kutambua umuhimu wa kutumia Nishati safi ya umeme kupikia, kutumia Majiko ya Umeme na kuachana na matumizi ya Kuni ambayo hupelekea athari za kiafya na uharibifu wa mazingira.

Akizungumza katika Maonesho ya Biashara na Utalii yanayoendelea katika viwanja vya Usagara, Mkoani Tanga, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Tanga, Mhandisi Mathias Solongo amesema moja wapo ya elimu inayotolewa katika Banda la TANESCO, ni pamoja na umuhimu wa kutumia Nishati safi ya umeme kupikia.

Amesema, “tunatoa elimu ya matumizi Bora ya Umeme, ikiwemo matumizi ya Umeme kwenye kupikia kama Nishati safi, kuna Majiko mbalimbali yapo hapa na mengine ni sufuria kabisa, hivi vyote tumevileta hapa kama mfano tu wa namna gani unaweza kutumia Nishati safi ya Umeme kupikia, bila kutumia Umeme mwingi na hivyo kupunguza gharama.”

Aidha, Mhandishi Solongo amewashauri wateja wa TANESCO na Wananchi kwa ujumla ambao wanataka kujiunga na huduma ya Umeme kutumia Mfumo wa Nikonekt ukaowawezesha kuomba huduma ya umeme popote.

“Sasa huduma zetu zinapatikana kiganjani kwako kupitia simu Yako ya mkononi, huna haja ya kuja mpaka TANESCO, huduma zetu zipo karibu na wewe, na kama unachangamoto juu ya matumizi ya Nikonekt ukaribu sana kwenye Banda letu tutakuelekeza na utaanza kufurahia huduma hii,” alisema.

Naye Mkazi wa Mkwakwani, Mariam Mbwana ambaye alitembelea Banda la TANESCO katika maonesho hayo amesema kuwa amepata elimu ya kutosha na kuwa Sasa ataanza kutumia Umeme kupikia kwani amekua akitumia gharama kubwa katika matumizi ya Mkaa.

 

TANESCO inashiriki maonesho ya biashara Mkoani Tanga kwa lengo la kuwaelimisha Wananchi kuhusu utoaji wa huduma, kutangaza Miradi ya kimkakati katika Sekta ya Nishati inayotekelezwa.

Watumishi Housing wang'ara tena tuzo za ACOYA
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Juni Mosi, 2024