Boniface Gideon -Tanga.

Huduma  mpya ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii nchini – NSSF wa NSSF Taarifa imetajwa kuwa ni muhimu kwa sababu inamuwezesha Mwanachama kupata taarifa binafsi, michango na madai yake.

Hayo yamebainishwa na Afisa Matekelezo Mkuu wa NSSF Mkoa wa Tanga, Abubakari Soud Mshangama katika maonesho ya 11 ya Biashara na Utalii, yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, Jijini Tanga huku akidai huduma hiyo inapatikana kupitia simu ya kiganjani kwa njia tatu ambazo ni ujumbe mfupi (SMS), Programu ya simu ya Kiganjani (Mobile App) ya NSSF na WhatApp.

“Leo tupo hapa kwenye maonyesho haya pamoja na kutoa elimu kuhusu huduma zetu lakini pia tunatumia kuitangaza Programu hii inamuwezesha mwanachama kupata taarifa na huduma mbalimbali kwa njia ya ujumbe mfupi, tumekuwa tukieleza mafao yanayotolewa na Mfuko na vigezo vyake ikiwemo Mafao ya Pensheni ya Uzeeni ambayo mwanachama hulipwa kila mwezi kwa anayetimiza vigezo vilivyowekwa.”

Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu wa Matekelezo Mkoa wa Tanga wa Mfuko  wa Taifa wa Hifadhi za Jamii NSSF, Abubakari Soud Mshangama.

Awali akizungumza mara baada ya kutembelea Banda la NSSF Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Zainab Abdallah amewataka wafanyakazi na wasiowafanyakazi kujiunga na mfuko huo, ili kuweza kunufaika na mafao mbalimbali ikiwemo ya matibabu.

Amesema wanapoweka akiba yako inakuwa ni rahisi unapokumbana na changamoto mbalimbali inakuwa ni rahisi kuweza kukuhudumia na kukupa matibabu ikiwemo unapofikia umri wa kustaafu unaweza kuwa na akiba yako ambayo inaweza kukulea mwenyewe.

 

Tanga: TRA yaendelea kutoa elimu kwa mlipa Kodi
Mfumo endelevu uboreshaji mafao, pensheni mbioni kukamilika