Tafiti na bunifu zinazoendelea kufanyika Nchini, zinalenga kuujulisha umma matokeo na kutoa majibu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya Watanzania, kama ilivyotatuliwa kero ya Maji kwa Wanawake, kupitia kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani.

Kauli hiyo, imetolewa hii leo Juni 5, 2024 na Naibu Waziri wa Maji, Kundo Mathew ambaye amemuwakilisha Waziri wa Maji, Jumaa Aweso katika maadhimisho ya Tisa ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu, iliyofanyika katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema, matokeo ya utafiti husaidia kupata majibu ya changamoto, na kutoa fursa kwa watanzania wengi kupata ajira na kuboresha hali za kiuchumi za watanzania wengi na ni msukumo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassa anbaye aliona zinatoa majawabu.

“Ni mpango wa Rais Samia kupitia Wizara ya Maji kuleta teknolojia mpya ya kutumia mita za kisasa (smart pre paid water meter), ili kuondoa kero ya watanzania kubambikiwa bili kubwa za maji, Upotevu wa maji kutokana na uchakavu na uzamani wa mita na kumsaidia mtanzania aweze kulipia maji kadri atumiavyo,” alisema Kundo.

Maadhimisho hayo, yebeba ujumbe usemao “Kukuza utafiti na ubunifu kupitia ubia baina ya chuo kikuu cha Dar es Salaam na Tasnia mbalimbali.”

Wakenya hawajatuzidi, ila wametuwahi: Idris Sultan
Wananchi wapewa darasa ununuzi Hati Fungani