Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt. Thomas Bwana ametoa Wito kwa Wadau wa Kilimo na Biashara kutembelea Banda la TARI kujifunza fursa za kibishara na Uwekezaji katika mnyororo mzima wa thamani wa Kilimo.
Dkt. Bwana ametoa Wito huo hii leo Julai 3, 2024 katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Kueleza hilo, Dkt. Bwana amesema Teknolojia za uongezaji thamani katika Mazao mbalimbali yanayofanyiwa Utafiti katika vituo vya TARI inafungua fursa kwa wajasiriamali kujiongezea kipato pasina ulazima wa kujishughulisha na Kilimo.
Dkt. Bwana anataja Teknolojia kama utengenezaji wa Mkate wa unga wa Mhongo, utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kutokana korosho kama mvinyo wa Bibo la Korosho pamoja na mvinyo wa Zabibu ambazo ni Teknolojia zinapatikana katika vituo vya TARI.
Pia Dkt. Bwana amesema fursa ya utoaji mafunzo kwa Wakulima wazalishaji Mbegu bora za Muhogo ikiwemo Mbegu bora za Mihogo zisizoshambuliwa na magonjwa ya batobato na Michirizi kahawia zinatoa fursa ya kibiashara kwa Wakulima na wajasiriamali huku akisema elimu hizo zote katika msimu huu wa maonesho zinatolewa katika Banda la TARI.