Johansen Buberwa – Kagera.
Chuo kikuu Dar es Salaam tawi la Kagera kimezindua mfumo mpya wa Sema pamoja na kukabidhi vifaa kwa kamati ya ujenzi utakaowezesha kupokea maoni pamoja na ushauri wa ujenzi wa mradi wa chuo hicho.
Mfumo huo umezinduliwa na Naibu Mratibu wa mradi wa chuo hicho, Dkt. Liberato Haule katika ahalmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini Mkoani Kagera, wakati wa semina iliyoandaliwa na chuo hicho kwa kamati ya ujenzi, viongozi wa Halmashari, Viongozi wa kata ya Karabagaine na Viongozi wa Vijiji vilivyopo kwenye kata hiyo.
Amesema, mfumo huo utasaidia kukusanya maoni pamoja na kupata taarifa juu ya ujenzi,ulinzi na usalama pamoja na hujuma zozote amabazo zinazoweza kutokea wakati wa mradi huo unapo endelea kutekelezwa kwa kipindi cha miezi 18 ambao umegharimu dola milioni 8.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba Vijijini, Fatina Laay ameishukuru Serikali kwa ujio wa ujenzi wa chuo hicho uliofikia hatu nzuri ya kuwapatia vifaa vya kutolea maoni kamati ya ujenzi na kuaidi ofisi yake ipo tayari kutoa msaada wowote utakao hitajika.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Privatus Moleka amesema kwa sasa wananchi wa kata Jirani ikiwemo Bujugo ndani ya halmashauri hiyo tayari wamesha anza kupokea wageni wanao hitaji kuwekeza kwa kununua aridhi ili kuongeza furusa na maendeleo kwa uchumi wa nchi.
Awali, Mwenyikiti wa Kamati ya Ujenzi, Charlse Kamando alisema mafunzo waliyoyapata yatawasaidia namna ya kutatua changamoto mablimbali kwa kutumia vifaa walivyopokea ikiwemo vitabu aina tano, ambavyo vitakuwa vinawaonesha mtiririko wa maoni kutoka kwenye jamii namnaya ya kutatua na mengine kufikisha kwenye ngazi za juu na vingine kuwasaidia kutunza kumbukumbu kwenye vitabu hivyo.