Johansen Buberwa – Kagera.

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanza kutafuta vipaji kupitia michezo mbalimbali inayoendelea, zikiwemo ndondo Cup, ili kukuza vipaji, ajira, ushirikiano pamoja na mahusiano.

Naibu Waziri Wizara ya utamaduni,sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma ameyasema wakati akizindua ligi ya Byabato Cup ya Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini, Wakili Stephano Byabato Mkoani Kagera.

Amesema serikali kwa sasa imetambua umuhimu wa michezo ikiwa ni njia moja wapo ya kuboresha afya na kuoneka kama kazi nyingine maana vijana wengi wameajiriwa katika sekta za burudani na michezo kupitia hapo wemekuwa matajiri wakubwa jambo ambalo linakuza uchumi na maendeleo ya Nchi.

“Mhe. Rais ametupatia kazi hiyo ya kusaka vipaji kote nchini niwahakikishie kwenye ligi hii nitaleta skauti hapa ili kuangalia vijana wenye vipaji na tuhakikishe tunawapeleka kwenye timu kubwa waweze kuhudumia nchi hii”amesema Naibu Waziri Mwijuma.

Katika hatua nyingine Naibu waziri Mwijuma amesema mwaka 2027 Tanzania inaadaa mashindano ya Afcon kwa kushirikiana na nchi za Kenya na Uganda.

Amesema, “kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi tunafanya marekebisho mkubwa kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa,Amani na tunajenga uwanja wa Samia Suluhu Hassan Arusha huku tutaendelea kufanya marekebisho katika viwanja mbalimbali na mchakato huo utafika kaitaba stadium kwa juhudi za Rais Samia.”

Ligi ya Byabato Cup imeanza kutimua vumbi Julai 6, 2024 ikishirikisha timu 14 za kata zote mechi ya awali ilikutanisha timu za wanawake Victoria Queen’s dhidi ya Omiseta Queen’s mpaka dakika tisini zinatamatika za maamuzi wa kati Geturuda Gerevazi zimetoka sale ya goli mbili na Mchezo wa ufunguzi wa jioni umekutanisha timu ya Bilele na Bakoba.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini wakili, Stephano Byabato amemshukuru Naibu Waziri Hamis Mwijuma kwa kuzindua ligi hiyo ambayo itakuwa msaada mkubwa wa kichocheo cha michezo kwa wakazi wa Bukoba.

Mfuko wa pamoja: Sillo awapa tano Wanahabari Manyara
Dkt. Feleshi aipongeza OSHA usimamizi sheria mahala pa kazi