Johansen Buberwa – Kagera.
Familia zilizoguswa na Mradi wa ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi Mkoani Kagera unaohusisha nchi za Afrika Mashariki wa (ECOP) utakaokuwa unasafirisha mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongeleani Mkoa wa Tanga nchini Tanzania zimeendelea kujengewa uwezo wa namna ya kujikimu kimaisha katika Kilimo, ufugaji na Biashara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo Wilayani Muleba Mkoani Kagera Haji Kihwele ambaye ni Kiongozi wa timu ya mipango wa urejeshaji wa hali ya kimaisha ya walioguswa katika mikoa ya Kagera na Geita amesema afua hiyo ya saba imekutanisha viongozi mbalimbali wa kiserikali.
Viongozi hao ni kuanzia ngazi za Vijiji, Vitongoji Halmashauri, Mkoa, watekelezaji pamoja na walioguswa wa bomba la Mafuta ghafi na mradi huo umelenga hali ya urejeshaji wa Mali kwa familia zilizoguswa katika zoezi la utoaji wa Ardhi, ili kupisha mradi huo.
Kwa upande Chartes Shagi ambaye ni Mratibu wa Uhusiano wa Jamii wa mradi wa mafuta ghafi (ECOP), amesema kuamzishwa kwa Mradi huo nchi ya Uganda bomba litakuwa na urefu wa kilometa 296 na Tanzania Bomba latakuwa na urefu wa kilometa 1147 na ambapo Mkoa nane itanufaika,wilaya 24 Halmashauri 27 na Mkoa wa Kagera utapita kwenye Halmashauri nne.
Amesema walioguswa wa Mradi huo kwa Kagera ni Watu 2196 katika Wilaya nne za Misenyi, Bukoba, Muleba na Biharamulo katika Wilaya inayoongoza ni Muleba yenye jumla ya kaya 1209 qmbqpo katika maeneo waliyokuwemo wanatarajia kujenga miundombinu saidizi katika wilaya za Misenyi na Muleba na kujenga kituo cha musukuma mafuta.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa ameshukuru kwq mradi huo wa mafuta ghafi kwa kutenga muda wa kutoa elimu ya Biashara kwa walioguswa na muradi kwa kurejesha hali ya Mali kwa waguswa katika Wilaya ya Muleba.
Amesema mbinu hizo za Biashara zitakuwa msingi wa kuboresha rasilimali tunazozalisha na kuwa faida zikiwemo ufugaji mbalimbali pamoja na nyuki,Kilimo na matarajio yake kutoka wa waguswa kufanikiwa kwa kupata tija,kuinuka kiuchumi na kimaendeleo kutokana na elimu waliyoipa.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa pia ametoa wito kwa viongozi wa dini kuwa mstari wa mbele kuwahubiria waumini wao kuchangamkia fursa za kibiashara.