Rais wa Marekani, Joe Biden ametambulisha kimakosa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy kama ‘Rais Putin’ “katika mkutano wa NATO unaofanyika jijini Washington kabla ya kujirekebisha mwenyewe akisema “Nimemakinika sana kuhusu kumpiga Putin.”

Alhamis ya Julai 11, 2024 Rais Joe Biden pia alichanganya majina ya Makamu wake Kamala Harris na mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump, huku akimuita Kamala jina la Trump, lakini akasisitiza kwamba anasonga mbele na azma yake ya kugombea tena kiti hicho licha ya kwamba Wademokratic wenzake wengi walimtaka asitishe kampeni.

Biden mwenye umri wa miaka 81, alizungumzia uzoefu wa miongo kadhaa kwenye jukwaa la dunia huku akisema kwamba alikuwa na sifa za kipekee kumshinda Rais wa zamani Trump mwenye umri wa 78, na kuiongoza Marekani kwa muhula mwingine wa miaka minne.

Tangu utendaji wake duni dhidi ya Trump katika mdahalo wa urais wiki mbili zilizopita, Biden amekabiliwa na mashaka yanayoongezeka kutoka kwa wafadhili, wafuasi na Wanademokrasia wenzake kuhusu uwezo wake wa kushinda uchaguzi wa mwezi Novemba na kuendelea na kuendelea kutekeleza kazi yake ipasavyo.

Mbinu bora KKK: Dkt. Msonde akutana na ujumbe wa USAID
Kagera: Walioguswa na mradi wapewa mbinu kuboresha maisha