Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Kenya, imesema Rais William Ruto amekubali kujiuzulu kwa Mkuu wa Polisi nchini Kenya, Inspekta Jenerali Japhet Koome.
Nafasi hiyo ya Inspekta Jenerali wa Polisi sasa inakaimiwa na Douglas Kanja ambaye alikuwa naibu wake, huku Rais Ruto akiwateua manaibu wawili watakaokaimu nafasi ya naibu inspekta jenerali, ambao ni Eliud Lang’at na James Kamau.
Ruto pia amefanya mabadiliko katika uongozi wa Magereza kwa kumfuta kazi John Wariouba ambaye inadaiwa alichukua likizo ya lazima kabla ya muda wake kuisha ambapo sasa Mkuu mpya wa Magereza nchini Kenya amekuwa Patrick Mwiti Arandu.
Hatua hii, inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Rais Ruto kutengua baraza la mawaziri nchini humo na mabadiliko hayo ni sehemu ya ahadi ya Ruto aliyoitoa kwa wananchi baada ya shinikizo la kutakiwa kufanya mabadiliko serikalini, ikiwemo yeye mwenyewe kujiuzulu.