Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua jengo la ofisi ya kamanda wa Polisi amesema Serikali itaboresha majengo yote Nchini.

Dkt. Samia ametoa kauli hiyo hii leo Julai 14, 2024 mkoani Katavi akiwa katika ziara yake ya kikazi ambapo Jengo hilo la kisasa limegharimu kiasi cha Bilioni 1.4 mpaka kukamilika.

Amesema “jengo la namna hii tumejenga maeneo mbalimbali Nchini na yanayofanana kama hivi, pia tuna kazi yakuboresha vituo vyote vya Polisi nchini.”

Rais Samia ameongeza kuwa, Serikali inafanya hivyo kulingana na mapendekezo ya tume ya kamati ya Jinai pamoja na Ilani inayotaka jeshi la polisi liwe na utulivu ili lifanye kazi yake ipasavyo.

Rais Samia: Waacheni Watoto wakue, wasizae Watoto wenzao
Katavi haina matukio mengi ya kiuhalifu - Rais Samia