Tanzania bado inatajwa kuwa na kiwango cha juu cha mimba za utotoni kwa kulitazama hilo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Julai 14, 2024 wakati ana kagua maendeleo ya Hospitali ya Rufaa Mkoani Katavi ameonekana kutopendezwa na idadi ya watoto waliochini ya miaka 18 kuingia katika vyumba vya kujifungua (leba) baada ya kupewa Ujauzito.
Amesema, “nimekuta mmoja tu ndio mpevu , Kwenye wodi watoto kuanzia miaka 15 -19 hakuna 20 ni mmoja tu 25 hawa watoto ndio wanajifungua watoto wenye matatizo niwaombe angalau mtoto anajifungua ni kuanzia miaka 19 huko mpaka 20, Waacheni watoto,Wakue kidogo kuzaa watoto wenzao waacheni waende shule.”
Takwimu zilizotolewa Mei 25, 2022 na shirikia lisilo la Kiserikali la Haki Elimu, zilionesha idadi ya Wanafunzi walioacha shule kutokana na mimba kupungua kwa asilimia 12.8 hapa nchini