Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan apokelewa kwa kishindo na Wananchi wa Kata ya kibaoni Halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele Mkoani Katavi, akitokea Manispaa ya Mpanda.

Mpimbwe ilimpokea Rais njiani katika mkutano waliouandaa ulioambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mizengo Pinda, Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu waziri wa ardhi nyumba pamoja na makazi, Geophrey Pinda, Mawaziri Viongozi wa Chama pamoja na Wananchi.

Hata hivyo, haya yanajiri baada ya Rais kumaliza ziara yake ya kikazi mkoani Katavi na hapa akiwa njiani kuelekea Mkoa wa Rukwa katika muendelezo wa ziara ambayo kimsingi ameamua kuzungumza na Wananchi na kukagua miradi ya kimaendeleo.

Uchaguzi wa Urais: Wanyarwanda wanaamua hatma yao hii leo
FEMATA waomba bei elekezi tozo kwa Wachimbaji wadogo