Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo ameshiriki Mbio za Mwenge wa Uhuru ambao umewasili mjini Babati.

Mbio hizo ambazo zinaongozwa na Kiongozi wa Kitaifa, Godfrey Mnzava, zimeanza hii leo Julai 15, 2024 ambapo utakagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2024 zimebebwa na Kauli Mbiu isemayo;- *Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa endelevu.*

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Julai 16, 2024
Rais Samia aelezea jitihada za kuufungua Mkoa wa Katavi