Mkaguzi Kata ya Ngara Mjini, iliyopo Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Olipa Chitongo amewaomba watoto kutoa taarifa za watu wanaowafanyia ukatili huku akibainisha kuwa wakifanya hivyo watapata maendeleo katika Masomo yao.
Mkaguzi huyo amebainisha hayo wakati akiongea na watoto wa kata hiyo ambapo aliwaomba kuwapa taarifa wazazi na walezi wao juu ya vitendo vibaya ambavyo watafanyiwa, huku akiwata pia kuwapata taarifa viongozi wa dini pamoja na Polisi, ili wachukuliwe hatua kali.
Aidha amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia kupungua na kuwabaini wale wote wanaowafanyia ukatili watoto ambapo alisisitiza kuwa ukatili umekuwa chanzo cha kudumaza maendeleo ya watoto kitaaluma.
Sambamba na hilo Mkaguzi Chitongo pia amewaomba wazazi wa kata hiyo kuwa karibu na watoto ili kuzifahamu changamoto wanazopitia nakuzitatua changamoto wanazozipitia watoto zikiwemo za ukatili.