Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Shule ya Wasichana Mkoa Rukwa katika kijiji cha Mtindilo Laela na Kuwasalimia Wanafunzi ikiwa ni sehemu ya Ziara yake Mkoani humo hii leo Julai 17, 2024.
Katika Mradi wa kutengeneza shule za Sekondari Nchini za Wanawake, Serikali ilitenga kiasi cha Bilioni 106.6 na mpaka sasa kimetumika kiasi cha Bilioni 104.4.
Kwa ujenzi wa shule hiyo ya mkoani Rukwa Mpaka sasa Serikali imetoa kiasi cha Bilioni tatu huku fedha nyingine zikitarajiwa kuwasilishwa.
Rais aliagiza kwenye mikoa 26 nchini kila mmoja ujenzi wa shule moja ufanyike na mpaka sasa shule 25 zimejengwa.