Mtu mmoja mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Shaban Adam (54), anashikiliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini – DCEA, akituhumiwa kutengeneza dawa za kulevya.

Adam alikamatwa nyumbani kwake Manzese Kilimani Juni 11, 2024 akitengeneza dawa za kulevya alizozitambulisha kama heroin kwa kutumia dawa tiba zenye asili ya kulevya akichanganya na kemikali bashirifu.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa baada ya kuzitengeneza dawa hizo huzisafirisha kwa kutumia mabasi ya abiria kama vifurushi kwenda mikoa mbalimbali nchini huku akisema siku za nyuma alikuwa akitengeneza dawa hizo za kulevya katika nchi za bara la Asia kwenye magenge ya wazalishaji wa dawa za kulevya.

Aidha, mtu huyo pia alitumika kama mbebaji wadawa hizo (punda) na aliporejea nchini aliendelea na uhalifu huo, huku DCEA ikieleza kuwa tayari imekamilisha kanzi data ya wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya na imeanza uchunguzi juu ya watu hao, wengi wamebainika kuwapo ndani ya nchi na nje ya nchi.

DCEA imefafanua kuwa baadhi yao huwa na biashara nyingine halali lakini wanajihusisha na biashara ya  na awa za kulevya na kufanya utakatishaji huku ikitoa wito kwao kuachana mara moja na biashara hiyo na kwamba uchunguzi dhidi yao unaendelea.

Sumbawanga: Bilioni 20.3 zajenga barabara kupendezesha mji
Waacheni wajifunze muda wao bado - Dkt. Samia