Serikali ya awamu ya sita chini Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 20 na Milioni 300 kwaajili ya kuanza Ujenzi wa Barabara kwa Km 13 za lami za kupendezesha Mji wa Sumbawanga

Hayo yamethibitishwa hii leo Julai 17, 2024 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Rukwa katika Uwanja wa CCM Mandera Mazwi na Mkuu wa mkoa huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere ameishukuru Serikali kwa kazi hiyo kubwa ya Ujenzi huo na amekiri endapo zitakamilika basi Mji wa Sumbawanga utabadilika.

RC Makongoro pia amessma Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wamempa Rais Samia zawadi ya  Ngo’mbe wanne na Mbuzi Wanne kwa kuthamini mchango wake.

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa pia amesema Ofisi yake ya Mkuu wa Mkoa nayo imemzawadia pia Ng’ombe wawili Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Bandari ya Kasanga kupunguza mrundikano wa Malori Tunduma
Ashikiliwa kwa kutengeneza, kusambaza Dawa feki za kulevya