Wazee wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kudhibiti vitendo vya kihalifu kwa baadhi ya vijana Mkoani Arusha, ambao wana tabia ya kutumia vibaya Pikipiki za magurudumu mawili na kutovaa kofia ngumu ambazo zitawaepusha na madhara makubwa pindi ajali itakapotokea.

Rai hiyo imetolewa na Koplo Sheilah Mwakaleja kutoka Dawati la Elimu ya Usalama Barabarani kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha alipotembelea katika kijiwe kimoja cha kahawa Jijini humo.

Koplo Sheila ametoa elimu kwa wazee hao juu ya madhara makubwa ya ajali zinapotokea kutokana na matumizi mabaya ya pikipiki ambapo amebainisha kuwa endapo msisitizo utaanzia nyumbani katika matumizi sahihi ya vyombo hivyo na kufuata sheria za usalama Barabarani ajali zitapungua kama sio kuisha alisema Koplo Sheila.

 

Aidha, amewaomba wazee hao kufika katika ofisi za Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha hususani dawati la elimu kupata elimu zaidi ya Usalama Barabarani ili kufikia hazima ya dawati hilo ya kumaliza ajali kupitia elimu inayotolewa na dawati hilo.

Amesema, endapo wazee hao watakuwa msatari wa mbele kuwaonya vijana katika matumizi mabaya ya pikipiki wategeme uchumi kukua na vijana wao kuendelea kiuchumi.

Rais Samia asisitiza suala la ulipaji kodi
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Julai 18, 2024