Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo asimamie shughuli zote za matibabu ya mtoto mwenye ulemavu wa mguu.

Mtoto huyo, ni yule aliyejitokeza hii leo Julai 18, 2024 katika mkutano wa njiani wakati Rais Samia  akiwasalimia Wananchi wa Tunduma akielekea Dodoma, mara baada ya kumaliza ziara yake Mkoani Rukwa.

Rais Samia amesema gharama zote za matibabu kumhusu mtoto huyo zitakua chini ya ofisi yake na kama kutakua na hoja ya kuletwa Dar es Salaam basi apelekwe haraka kwa ajili ya matibabu.

Kenya: Polisi yapigwa marufuku maandamano
Simbachawene: Marufuku kuwasumbua Watumishi