Mkaguzi kata ya Oldonyosambu Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Hamisi Malegea amewaomba Wananchi kushiriki kikamilifu katika masuala ya ulinzi pamoja na maendeleo ya kata hiyo.

Rai hiyo ameitoa wakati wa kikao cha Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, Emmanuel Oleshangai ambapo Mkaguzi huyo amewaomba wananchi hao wa jamii ya kifugaji kutambua kuwa suala la ulinzi ni la wote kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kukomesha uhalifu katani hapo.

Aidha amewaomba kuendelea kuviboresha vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo amebainisha kuwa kwa kutambua jamii hiyo kuwa ya kifugaji vitasaidia suala la ulinzi wa mifugo yao.

Ameongeza kuwa endapo kutakuwa na kutamaduni wa kupeana taarifa za uhalifu baina ya kaya na kaya basi watambue kuwa suala la uhalifu katani hapo litakuwa historia.

Vilevile amewaomba Kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili hatua sitahiki ziendele kuchukuliwa kwa ambao watabainika kuhusika na vitendo vya kiuhalifu.

Kisa mafuriko: Wapendekeza mji mkuu uhamishwe
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Julai 23, 2024