Msemaji wa Polisi Nchini Uganda, Kituuma Ruspke amesema wanawashikilia wabunge watatu na watu wengine saba, ambao walikamatwa na kuwekwa rumande katika mkesha wa maandamano yaliyopigwa marufuku na serikali wakipinga ufisadi.

Ruspke amesema wote kwa pamoja watafikishwa Mahakamani kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukiuka sheria za barabarani, tukio ambalo linajiri siku chache baada ya Rais Yoweri Museveni, kuwaonya wanaopanga kuandamana akisema wanacheza na moto.

Amewataja Wabunge hao kuwa ni Francis Zaake, Charles Tebandeke na Hassan Kirumira, wote wa chama cha upinzani cha National Unity Platform – NUP na watafikishwa mahakamani Julai 25, kwa ajili ya kusikilizwa shauri lao la kuachiwa kwa dhamana.

Hata hivyo, Waandamanaji waliapa kuendelea na maandamano yao ya kupinga ufisadi, wakipata msukumo wa maandamano ya kuipinga serikali yaliyotarajiwa kuendelea hii leo katika nchi jirani Kenya.

Wasiowapeleka Watoto shule kuchukuliwa hatua
Hukumu nyepesi kwa wanaobaka Watoto zalalamikiwa