Serikali nchini, imesema itawachukulia hatua wazazi wote wasiowapeleka watoto wao shule ili waweze kupata haki yao kielimu.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Ilyamchele Kata ya Namonge Wilayani Bukombe Mkoani Geita.
Amesema, Wazazi wanatakiwa kuhakikisha wanawapeleka Watoto wao shule na wale wanaoleta ukinzani dhidi ya maelekezo hayo waripotiwe katika ngazi husika, ili kutafuta suluhu ya tatizo hilo.
Aidha, Dkt. Biteko akiwa katika eneo hilo pia alijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa, ikiwemo kuelekeza kufanyika kwa ukarabati wa Zahanati ya Kijiji hicho, ili kumaliza kilio cha kukosa huduma za kiafya.