Angela Msimbira, Nzega – Tabora.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Zainab Katimba amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuzingatia utengaji wa bejeti kupitia mapato ya ndani ili kuendeleza miundombinu ya sekta ya elimu.

Katimba ametoa melekezo hayo alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Tabora kwenye eneo la ekari 23 litakalotumika kujenga shule ya amali katika Halmashauri ya Mji Nzega.

Amesema mamlaka za serikali za mitaa zina wajibu wa kuhakikisha zinaendeleza miundombinu ya elimu na kutoacha jukumu hilo kwa serikali kuu pekee.

 

“Pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na Mheshimiwa Rais Samia kuleta fedha nyingi za kutekeleza miradi katika sekta ya elimu ili kuhakikisha wanafunzi wetu wanapata elimu iliyobora, sasa mamlaka za seriali za mitaa zisiache jukumu la kuendeleza miundombinu iliyofanywa na Serikali kuu pekee bali jukumu la msingi ni la mamlaka za serikali za mitaa,” alibainisha Katimba.

Akizungumzia ziara hiyo, Katimba amesema ametembelea maeneo tofauti tofauti na kukagua majengo katika shule mbalimbali ikiwemo shule ya sekondari ya sayansi ya wasichana ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amepeleka Sh bilioni 4.1 na tayari imeshaanza kuchukua wanafunzi.

Amesema, “katika ukaguzi wa miradi hii katika sekta ya elimu tumepita na tumetizama miundombinu imara tumeshuhudia jitihada kubwa iliyofanywa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anashusha fedha nyingi sana kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu.”

Aidha ameongeza kuwa, kutokana na juhudi hizo za Rais Samia, watanzania wanapaswa kujua kuwa wanajukumu la msingi la kuendelea kuchangia katika kustawisha mazingira mazuri zaidi ya wanafunzi kupata elimu.

Othman ahimiza maadili kuvutia jamii ushiriki wa michezo, mazoezi
Mfumo GOTHOMIS: Wadau wahimizwa kuongeza ufadhili