Shambulizi la Israel katika shule moja iliyopo Deir al Balah huko Ukanda wa Gaza, limesababisha vifo vya Wapalestina 30 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa, huku Jeshi la Israel likisema ni. ahati mbaya kwani lilinuia kukilenga kituo cha Hamas.

Kufuatia mkasa huo, Jeshi la Israel limewataka wakazi wa mji huo wa kusini wa Khan Younis kuondoka eneo hilo baada ya kuopoa miili ya Waisraeli watano.

Aidha, pia Jeshi hilo limeonya kuhusu mashambulizi mapya hukuUmoja wa Mataifa ukisema zaidi ya Wapalestina 180,000 tayari wamekimbia mapigano katika eneo hilo.

Tukio hilo linajiri wakati ambapo shirika la ulinzi wa raia wa Gaza likisema operesheni ya kijeshi ya Israel iliyoanza mapema wiki hii katika mji wa Khan Younis imeua takriban watu 170 na kuwajeruhi mamia huku dadi ya vifo Gaza ikifikia watu 39,258.

Rais Samia: Mshirikiane kutatua changamoto za kidunia
Serikali yataka michango isiwazuie Watoto kupata elimu