Vilabu mbalimbali vinavyoshiriki ligi kuu NBC kwa msimu wa 2024/25 vimeanza kunufaika na sajili walizofanya wakati huu wa majira joto. Klabu ya Simba wao wamesajili wachezaji wengi zaidi wa kigeni lakini pia Yanga wamezidi kuimarisha kikosi chao kwa kusajili wachezaji wazoefu waliowahi kuchezea timu mbalimbali za hapa nyumbani.

klabu ya Coastal Union wao wamezidi kufanya mabadiliko ndani ya kikosi chao kwa kusajili nyota wa tano,kuimarisha benchi lao la ufundi kwa kumuongezea nguvu kocha David Oouma. Kwa azam fc sote tumeshuhudia namna ilivyowaondoa wachezaji wake muhimu kama Kipre Junior na Ayubu Lyanga lakini pia tumeshuhudia namna walivyofanya usajili wa wachezaji hodari ili waweze kufanya vyema msimu huu.

Tunavigusia vilabu hivi vinne kwa sababu vitatuwakilisha katika michuano ya kimataifa . Azam na Yanga watashiriki ligi ya mabingwa Afrika wakati Simba na Coastal union watatuwakilisha katika michuano ya kombe la shirikisho.

Maandalizi ya Msimu mpya 

Azam FC 

Klabu ya Azam Fc iliweka kambi yake nchini Morocco na iliondoka nchini ikiwa imekamilisha usajili wa nyota  wote iliokuwa ikiwahitaji akiwemo jhonier blanco,franck tiesse,ever meza,Mamadou Samake,Adam Adam na Cheickna Diakite,. wakiwa nchini Morocco walicheza michezo dhidi ya Wydad Athletics mchezo uliomaizika kwa azam kupoteza kwa mabao4-1.mchezo mwingine dhidi ya Touarga uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya US Mansour. Azam imejipanga kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya APR ya nchini Rwanda tarehe tatu na itacheza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Coastal Union kombe la Community Shield tarehe 8.

Coastal Union 

Mara baada ya msimu kumalizika Coastal Union ilitangaza kuachana na nyota wake muhimu walioisaidia klabu hiyo kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi na kufika hatua ya nusu fainali ya kombe la CRDB. baadhi ya nyota waliopewa mkono wa kwa heri ni Ibrahim Ajibu Migomba,,Abubakari Abasi,Roland Beako,omary mbaruk,felly mulume,kocha msaidizi fikiri ,chrispin ngushi na ugando. na klabu hiyo ilifanikiwa kuwasajili nyota wapya akiwemo Abdallah Hassan ,Anguti Luis,Mbarak Yusuf ,Ramadhan MwendaMukrim Issa,Haroub Mohamed ,Athuman Msekeni na kocha msaidi kocha Ngawina Ngawina.

Coastal Union ilishiriki michuano ya Dar Port CECAFA na haikufanya vyema baada ya kucheza michezo mitatu ikipoteza mchezo 1 ,sare 1 na kufungwa mechi 1. kwa sasa timu hiyo imeweka kambi yake visiwani Pemba kujiandaa na mchezo wa nusu fainali ya kombe la community Shield dhidi ya Azam fc tarehe 8 na. Msimu wa 2024/25  itashiriki michuano ya kombe la shirikisho Afrika na imeonekana kujipanga vyema ili kufanya vyema .

Simba SC 

Klabu ya Simba haikiwa na wakati mzuri msimu wa 2023/23 baada ya msimu kumalizika ililazimika kuachana na nyota mbalimbali wa kigeni akiwemo Luis Miquissone,Babakar Sarr ,Clatous Chama, Saido Ntibazonkiza,Sadio Kanoute na Henock Inonga Bacca. Klabu hiyo iliingia sokoni na kuwasajili nyota wengine wa kigeni pamoja na nyota wa kitanzania ili kuweza kuimarisha kikosi chao kwa msimu ujao. Simba hawakuishia hapo tu bali walivunja benchi zima la ufundi na kumuajiri kocha mpya David Fadlu kutoka Afrika Kusini aliyewasili na benchi zima la ufundi .

Usajili wa benchi la ufundi na wachezaji umeanza kutoa matumaini kwa klabu hiyo baada ya kucheza michezo mitatu ya kirafiki na kupata ushindi wa michezo yote. nyota kama Mukwala na Mutslr esmrgruks gumzo kes mashabiki wa timu hiyo na wanaamini watafanya vyema kwenye michuano ya ligi pamoja na kombe la shirikisho.

Yanga SC

Mabingwa watetezi wa ligi ya NBC na kombe la CRDB waliweka kambi Avic town na walikwenda Afrika kusini kucheza michezo ya kujipima dhidi ya FC Augusburg mchezo waliopoteza kwa mabao 2-1 na kupata ushindi dhidi bao 1-0 dhidi ya TS Galaxy. Yanga iliushitua ulimwengu wa soka kwa kutwaa ubingwa wa TOyota Cup kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya waandaaji Kaizer Chief na kila mchezaji aliyeshiriki katika mechi hizo alikuwa gumzo kwa kiwango kizuri alichoonyesha.

Tarehe 4 Yanga watawakaribisha Red Arrows kwenye kilele cha wiki ya wananchi kisha tarehe 8 watacheza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba uwanja wa Benjamini Mkapa. Yanga hawajafanya usajili wachezaji wengi kwenye  kikosi chao bali wameongeza nyota wachache waliofanya vizuri msimu huu wakiwa na vilabu vyao. Usajili wa Prince Dube,Duke Abuya , Jean Baleke na Clatous Chama umezidi kuimarisha timu hiyo kuelekea michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika ,kombe la CRDB na michuano ya ligi ya kuu NBC.

Kwa sajili zilizofanyika kwa kila timu tunaamini timu hizi zitafanya vyema kwenye michuano ya kimataifa na hatimaye kuleta makombe ya Afrika nchini.

 

 

Chelsea yamnasa Golikipa Jorgensen
Tetesi za usajili Duniani Julai 31, 2024