Klabu ya Manchester United imejikuta njia panda baada ya beki wake mpya Lennie Yoro kukumbwa na majeraha yatakayomweka benchi kwa kipindi cha miezi 3. Beki huyo alikumbwa na majeraha hayo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Arsenal na taarifa kutoka kwa madaktari wa timu zimethibitisha kwamba nyota huyo mwenye miaka 18  hatocheza mchezo wowote mpaka mwezi Oktoba.

Lennie Yoro alisajiliwa kwa dau la paundi milioni 58 kutoka Lile ya ufaransa ili kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi ya Manchester United iliyokuwa ikiongozwa na Harry Maguire,Dalot,Martinez na John Evans.

Yoro atakosa michezo 9 ya mwanzo ikiwemo mechi dhidi ya Liverpool, Aston Villa na Tottenham.Majeruhi haya yatamfanya kocha Erik Ten Hag kuendelea kuwatumia mabeki wa zamani ambao walimfelisha.

Naye mshambuliaji Hojlund ataukosa mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Manchester City mchezo utakaopigwa dimba la wembley tarehe 10 agosti baada ya kukumbwa na majeraha katika mchezo dhidi ya Arsenal.

Marcus Rashford naye alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Real Betis uliomalizika kwa United kupata ushindi wa mabao 3-2 lakini pia winga  Antony aliondolewa uwanjani baada ya kupata maumivu ya mkono katika mchezo huo.

Manchester United itaanza kampeni zake za kuwania ubingwa wa Uingereza tarehe 16 Agosti dhidi ya Fulham na itashiriki michuano ya Europa na FA kwa msimu huu bila ya nyota hao wanne.

 

Dkt.Msonde ataka uadilifu, ufuatiliaji Miradi ya maendeleo
Aliyenyimwa haki ya elimu arudishwa shuleni