Leo Agosti 1, 2024, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anazindua rasmi wa treni ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) inayofanya safari zake kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.

Kabla ya uzinduzi huo, Rais Samia atafanya ukaguzi wa stesheni ya mkoa wa Morogoro na baadaye, kuzungumza na Wananchi wa Manispaa ya Morogoro katika viwanja vya stesheni hiyo.

 

Tayari Wananchi wa mkoa wa Morogoro wamekusanyika kwa wingi katika viwanja vya stesheni ya treni Morogoro, wakiwa na shauku ya kumkaribisha na kumsikiliza Rais Samia, huku wakitoa shukrani zao kwa serikali kwa jitihada za kuboresha miundombinu na huduma za usafiri nchini.

Treni ya SGR ni mradi mkubwa na wa kisasa uliofadhiliwa na serikali kwa lengo la kuboresha miundombinu ya usafiri nchini. Mradi huu unatarajiwa kupunguza muda wa safari na gharama za usafirishaji, hivyo kuboresha huduma kwa wananchi na kuchangia katika ustawi wa jamii na maendeleo ya uchumi wa taifa.

Wananchi wa Morogoro wanatoa shukrani zao kwa Rais Samia na serikali kwa jitihada zao za kuboresha miundombinu na huduma za usafiri nchini.

Uzinduzi wa treni ya kisasa ya SGR ni hatua muhimu katika juhudi za serikali ya Tanzania kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wake

TLS isimamie haki, amani kuchochea maendeleo: Dkt. Biteko
Arne Slott arejesha matumaini Liverpool baada ya ushindi dhidi ya Arsenal