Tuzo za TFF zimetamatika usiku wa jana kwa klabu ya Yanga kuibuka kinara wa tuzo hizo ikitwaa tuzo nyingi zaidi kuliko klabu yoyote. Klabu hiyo yenye makao makuu jijini Dar es salaam mitaa ya Twiga na Jangwani iliibuka kinara wa tuzo na kubwa zaidi ni ile ya kumtoa mchezaji bora wa msimu kwa mara ya tatu mfululizo.
Msimu wa 2021/22 mchezaji Yanick Bangala aliibuka kama mchezaji bora wa Msimu (MVP) Msimu wa 2022/23 Mshambuliaji Fiston Kalala Mayele alitangazwa mchezaji bora wa msimu(MVP) na msimu uliomalizika wa 2023/24 ulimtangaza bw.Stephen Aziz Ki kuwa mchezaji bora wa msimu kwa kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu NBC na kombe la CRDB FA CUP lakini pia kiwango kizuri alichokionyesha kwa kuwa kinara wa mabao NBC premier league ,ubora wake eneo la kiungo ndizo sababu zilizompa tuzo hiyo.
Klabu ya Yanga ilifanikiwa kutwaa tuzo za ( Mchezaji Bora NBC ,Mfungaji BoraNBC, Kiungo bora wa NBC zilizokwenda kwa Aziz Stephane Ki) Tuzo ya golikipa bora CRDB CUP iliyokwenda kwa Djigui Diara na Mshambuliaji Clement Mzize akiibuka mfungaji bora wa kombe la CRDB FA CUP, Ibrahim Bacca aliibuka na tuzo ya beki bora wa NBC ,Kocha Miguel Gamondi aliibuka ndiye kocha bora wa msimu . Klabu hiyo ilitoa wachezaji 6 walioingia kwenye orodha ya kikosi bora cha msimu ambao ni Dickson job, Ibrahim Hamad Bacca, Mudathir Yahya Kouassi Yao,Max Nzengeli na Aziz Ki.
Wachezaji wengine waliotwaa tuzo hizo ni Golikipa wa Coastal UnionLay Matampia aliyeingia pia kikosi bora cha msimu ,Mohammed Hussein wa Simba aliyeibuka beki bora wa msimu, Kiungo Feisal Salum alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa CRDB Federation Cup pamoja na kuingia kwenye kikosi bora cha msimu.
Orodha ya waliotwaa Tuzo.
Aisha Mnunka – Mchezaji bora na mfungaji bora (Tanzania Women Premier League)
Ayoub Masudi- Mchezaji bora First League
Jaruth Juma- Mchezaji bora soka la ukweni
Mbwana Samatta – Mchezaji bora wa Tanzania anayecheza nje kwa wanaume
Aisha Masaka – Mchezaji bora wa Tanzania anayecheza nje kwa wanawake
Kipre Emmanuel JR- Goli bora ligi kuu ya NBC
Leodeger Tenga -Tuzo ya Heshima
Said El Maamry – Tuzo ya raisi TFF
Juma Bomba- Tuzo ya heshima soka la wanawake
Caroline Rufo – kipa bora ligi kuu ya wanawake
Hamis Kitila -Kamishina bora ligi kuu NBC
Shomari Raheem – Mchezaji bora chipukizi ligi kuu NBC
Ahmed Arajiga -Mwamuzi bora ligi kuu ya NBC
Ester Maseke- Mchezaji bora chipukizi ligi kuu ya wanawake
Amina Kyando- Mwamuzi bora ligi ya wanawake
Zawadi Yusuph – mwamuzi msaidizi bora ligi kuu ya wanawake
Mohammed Mkono- Mwamuzi msaidizi bora wa ligi kuu ya NBC
Bunda Queens -Timu yenye nidhamu ligi kuu ya wanawake
Mtibwa sugar -Timu yenye nidhamu ligi kuu ya NBC