Ikiwa imebaki siku moja kwa klabu ya Simba kuifikia Simba Day na siku mbili kwa klabu ya Yanga kuhitimisha wiki ya Wananchi basi kuna mambo ambayo mdau wa michezo kupitia DAR24 hutakiwi kuyakosa kabisa. Wiki hizi mbili zimekuwa ni wiki za mapato makubwa kwa klabu hizi mbili za jijini Dar es salaam. Unaweza kujiuliza je vilabu hivi vimewezaje kuwa gumzo kwenye midia mbalimbali za ndani na nje ilihali havijacheza michezo yoyote mikubwa ya kiushindani?
Jibu lake ni rahisi kabisa Brand za SIMBA na YANGA ni Imani za watu wengi hapa nchini. Simba na Yanga zinatajwa kila mahali na ili tukio lako libambe iwe msiba au shangwe basi vitaje vilabu hivi ndipo utaamini ninachokwambia. Leo hii Simba na Yanga zinatajwa mpaka makanisani na misikitin,zinatajwa mpaka bungeni na ikulu na ni kama maisha ya kila mtanzania yapo hapo. Swali ni je kila wanachofanya Simba na Yanga kinaingiza pesa? na je pesa hizo wanaziingizaje?
WADHAMINI WA MATAMASHA
Kuelekea kilele cha Simba day na Wiki ya wananchi tumeshuhudia wadhamini mbalimbali ambao wamejitokeza kudhamini tukio hilo. Kama utapita katika akaunti za mitandao ya kijamii ya timu hizo utaona wamewaorodhesha wadhamini hao. Mabenki,mashirika ya umma na binafsi nayo yamezitumia klabu hizo kujitangaza. Ni hivi majuzi tumeshuhudia baadhi ya media zikikabidhiwa majukumu ya kulipa promo tukio hilo na nyingine kuonyesha tukio hilo kupitia runinga je unadhani ni kiasi gani vilabu hivyo vimepata?
MAUZO YA JEZI
Hapa ndipo panazungumziki zaidi kwani ndani ya wiki moja mauzo ya jezi za timu hizo yamekuwa makubwa mno. vilabu vimetajilika na wauzaji wa rejareja wamenufaika mno . Kwa sasa wasambazaji wa jezi za Simba na za Yanga wanashangilia kwani uwekezaji walioufanya umerudisha faida kubwa mno. Wabunifu wa mavazi hayo wamepewa maua yao na kila mtu amesifu kazi zao nzuri za kiubunifu. Kama mikataba baina ya wasambazaji na vilabu imefuatwa vyema basi klabu hizo zimetajirika mno ndani ya wiki moja.
MAUZO YA TIKETI ZA MATAMASHA
Klabu ya Simba ilimaliza mauzo yake ya tiketi elfu 60 siku 3 kabla ya tukio la simba day. bado hatujapata figa kamili ni kiasi gani klabu hiyo imekitengeneza kwa tukio la kesho lakini naamini ni pesa nyingi mno. Kwa upande wa Yanga na wao hawako nyuma kimauzo .Tiketi zote za gharama zimekwisha malizika na sasa wanamalizia zile za machungwa,mzunguko na VIP C kwa mauzo waliyoyafanya mpaka sasa naamini ni pesa nyingi na zitawafikisha mahala wanapopakusudia.