Klabu ya Azam FC imewasili jijini Kigali-Rwanda kwa mualiko maalumu kutoka kwa klabu ya Rayon Sports ya nchini humo. Rayon Sports wameandaa tukio la RAYON SPORTS DAY litakalofanyika siku ya kesho tarehe 3.Tukio hilo halitofautiani sana na lile la Simba Day na Yanga Day na litahusisha kutambulisha wachezaji wao wapya akiwemo Haruna Niyonzima aliyewahi kuzichezea Simba na Yanga.

Timu hiyo iko chini ya kocha Robertinho aliyewahi kuifundisha klabu ya simba mwanzoni mwa msimu wa 2023/24 kabla ya kufukuzwa baada ya Simba kupokea kipigo cha mabao 5-1 mwezi November 5 2024 kutoka kwa Yanga . pamoja na mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Azam FC. tukio jingine ni kutambulisha rasmi jezi zake mpya za msimu wa 2024/25 ambazo zimekwishaanza kuuzwa kwa kasi kubwa nchini humo kupitia maduka ya Rayon Sports Shop.

Mchezo huu ni muhimu kwa Azam FC na ni mchezo wake wa 4 wa maandalizi kuelekea msimu ujao. Azam FC watacheza mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Coastal Union katika hatua ya nusu fainali ya ngao ya jamii visiwani unguja katika dimba la New Amaan Stadium na kama watafika fainali basi watakutana na mshindi kati ya Simba au Yanga.

msimu wa 2024/25 ni muhimu kwa Azam kwani itashiriki michuano ya Ligi ya mabingwa Africa ,Ligi kuu NBC ,CRDB CONFEDERATION CUP na kuna uwezekano kushiriki kombe la mapinduzi visiwani zanzibar mwanzoni mwa mwezi Januari 2025

Kamanda Katabazi ahimiza michezo katika jamii
Hivi ndivyo Simba na Yanga zinavyopiga pesa ndefu nje ya uwanja