Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuiombea nchi dua na viongozi wake waendelee kudumisha amani, mshikamano utulivu kuelekea uchaguzi mkuu mwakani
Dkt. Mwinyi aliyasema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa Msikiti wa Rahman Taveta, Mkoa wa Mjini Magharibi hii leo Agosti 2, 2024.
Amesema hakuna maendeleo pasipokuwepo amani na utulivu na kwamba maombezi hayo pia yaelekezwe kwa viongozi ili waendelee kudumisha amani, mshikamano utulivu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani.