Waziri Mkuu wa Bangladesh, Sheikh Hasina, amejiuzulu na kukimbia nchi hiyo kufuatia maandamano makubwa yaliyokuwa yakimshinikiza kuchukua hatua hiyo ambapo Jeshi lilitoa amri ya kutotoka nje ambayo ilipingwa

Raia hao wenye hasira walikataa kutii amri ya kutotoka nje iliyotangazwa na jeshi la nchi hiyo na kuingia mitaani kumtaka Waziri Mkuu huyo kujiuzulu, ambaye  anasemekana amekimbilia nchini India.

 

Ilihofiwa kuwa ghasia za leo Agosti 5, 2024 zingeweza kuwa kubwa kuliko zilizoshuhudiwa siku ya jana, baada ya waandamanaji kukabiliana na wafuasi wanaoiunga mkono serikali, ambapo takribani watu 100 waliuawa wakiwemo maafisa 14 wa Polisi.

Hatua hii inafuatia maandamano ya Wanafunzi yaliyoanza mwezi uliopita wakitaka kusitishwa kwa mfumo wa ajira serikalini wanaodai ulikuwa na upendeleo na yalishika kasi na kugeuka kuwa machafuko mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika utawala wa miaka 15 wa Sheikh Hasina.

 

Serikali yawaalika wawekezaji Kilombero, Ulanga
Prof. Assad aongoza Kongamano ujenzi Hospitali ya Kiislamu