Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani, Juma Ndaruke amewataka Wakala wa Misitu Tanzania – TFS kutoe elimu ya umuhimu wa upandaji miti kwa jamii.

Ndaruke ameyabainisha hayo wakati Kamati ya siasa ya wilaya ya Kibiti ilipofanya ziara za kutembelea shughuli mbalimbali zinazofanywa na TFS Wilayani Kibiti na kutaka pia wahamasishe upandaji wa miti ya matunda, vivuli na mbao.

Amesema, Wananchi wa Wilaya ya Kibiti wanapenda zaidi kupanda miti ya matunda na vivuli, hivyo waieleze pia jamii kuhusu fursa mbalimbali zilizopo katika ufugaji nyuki, ili wanufaike kupitia eneo hilo.

“Kuna fursa katika ufugaji nyuki na wananchi wanatakiwa kujua fulsa hizo waambiwe waanze ufugaji wanufaike fanyeni mikutano wazi mkiwaaambia wananchi kuhusu fulsa hizo kwa kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya ufugaji nyuki,” alisema Ndaruke.

Naye Muhifadhi Mkuu wa Wakala huduma za misitu wa Wilaya, Devis Mlowe amesema mwaka 2023 walipanda miche laki 5 ya matunda, vivuli na mbao miche 434000 kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali ikiwemo taasisi za Serikali, Wananchi, Taasisi za dini, binafsi pamoja na Wilaya jirani za Mkuranga, Rufiji, Kibaha.

Rais Samia atembelea mabanda, aweka jiwe la msingi Nanenane
Rais Samia aweka jiwe la msingi ujenzi Maabara kuu ya Kilimo