Klabu za Manchester United na Manchester city zitavaana hapo Kesho kwenye mchezo wa fainali wa kombe la ngao ya jamii kwa msimu wa 31 tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.

Manchester United wanafikia hatua hizo baada ya kushinda ubingwa wa FA walioupata msimu wa 2023/24 kwa kuwafunga mahasimu wao Manchester city kwa mabao 2-1.Manchester city wametinga fainali hizo baada ya kuibuka na ubingwa wa ligi kuu uingereza msimu wa 2023/24.

Mchezo huo utapigwa dimba la Wembley jijini London na utafungua rasmi msimu wa 2024/25. Wachezaji wanaotegemewa kufanya makubwa katika mchezo huo ni Bruno Fernandez na Hojlund kwa upande wa Manchester United na Halaand pamoja na Kelvin Debruyne kwa upande wa Manchester city.

Mfumo wa michuano hii

Mfumo wa michuano hii umegawanyika katika vipengele viwili. Kipengele cha Kwanza kinasema bingwa wa FA atacheza mchezo wa Kombe la ngao ya jamii na bingwa wa ligi kuu uingereza.

Mfumo wa pili unasema :kama bingwa wa ligi kuu uingereza atatwaa pia Kombe la FA ndani ya msimu mmoja basi timu hiyo itacheza fainali ya Kombe la ngao ya jamii na timu iliyomaliza nafasi ya pili kwa msimu husika. Mfumo huu ulitumika msimu wa 2022/ 23 ambapo Manchester city  alitwaa makombe ya ligi na FA na katika msimamo wa ligi kuu Arsenal ndiye aliyeshika nafasi ya pili ndipo kanuni hii ilitumika na timu hizo zilikutana fainali ya ngao ya jamii.

Erik ten hag Vs Pep Guardiola

Kocha wa Manchester city amefanikiwa kuiongoza timu hiyo katika michezo 6 akipata ushindi wa mechi 4 na kupoteza mechi mbili. Guardiola amefanikiwa kuiongoza Manchester city kupata ushindi mkubwa wa mabao 6-3 dhidi ya Erik Ten hag msimu wa 2022/23. Kocha huyo hajawahi kupoteza mchezo wowote wa ligi dhidi ya Erik Ten hag.

Kwa upande wa Manchester United bw.ten hag amefanikiwa kushinda mechi mbili pekee  dhidi ya Guardiola.  Ten hag aliibuka bingwa wa FA dhidi ya Guardiola msimu wa 2023/24 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1

Mategemeo ya mchezo huo

Rekodi zinaonyesha Manchester United imekuwa Bora Sana katika michuano hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1908 ikitwaa Kombe hilo mara 21 wakati wapinzani wao Manchester city wakitwaa mara 6 pekee.

Mara ya mwisho kwa Manchester city kutwaa Kombe hilo ni mwaka 2023 na Manchester United wakitwaa Kombe hilo mwaka 2016.

Huu ni mchezo unaokwenda kufungua kurasa mpya ya kimashindano baina ya makocha hawa wawili.

 

Mradi EACOP kupewa msukumo
Simulizi: Sina hamu na Ukahaba