Serikali imesema tayari imekamilisha mipango kadhaa ya kupata fedha kwa kushirikiana na benk ya dunia Kujenga miundo mbinu ya kudumu katika maeneo yaliyoathiriwa na Mvua za elinino hapa nchini kwa mvua zilizoanza mwishoni mwa mwaka Jana Hadi mwanzoni mwa mwaka huu.
Naibu Waziri wa ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema hayo wakati alipofanya ziara ya siku moja kukagua maeneo yaliyokarabatiwa kwa muda baada kuathiriwa na mvua hizo kwa kuangalia tathimini iliyofanywa na Wataalamu ili kuanza kujenga miundombinu ya kudumu.
Alisema, Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa iliyoathirika sana na mafuriko hasa Barabara kubwa inayotoka Dar es salaam, mkuranga, Kibiti kwenda Hadi mkoa wa Lindi ambayo barabara zake zililazimika kutumika upande mmoja na Wataalamu wakarudisha hali ya kawaida kwa muda.
Alisema ametembelea eneo la Kimanzichana lililoathirika zaidi na mvua hizo za elinino, ili kujionea changamoto iliyokuwepo na kuangalia chakufanya ilikujenga miundombinu ya kudumu baada ya kilichofanyika awali baada ya Wataalamu kurejesha mawasiliano kwa muda ili Sasa ijengwe miundombinu ya kudumu.
Alisema Wataalamu walifanya tathimini na usanifu wa kurejesha mawasiliano ya kudumu katika eneo hilo ambayo mvua hizo zilisababisha Barabara kutumika upande mmoja katika kipindi kile cha mafuriko lakini Wataalamu walirudisha miundombinu hiyo kwa muda na kuendelea kutumia njia mbili.
Alisema kwakuwa kilichofanyika lilikuwa cha muda, Serikali ilitoa maelekezo kwamba Wataalamu wafanye tathimini ili kujenga miundombinu hiyo ya kudumu.
Akikagua ujenzi wa barabara ya Mkuranga-Kisiju KM 45 na barabara ya Kilwa mkoani Pwani amehimiza ushirikishwaji wa Wananchi katika kulinda hifadhi ya barabara ili kuepuka uvamizi wa hifadhi hizo hali inayosababisha uchimbaji wa mchanga na mawe na hivyo kuathiri barabara na madaraja wakati wa mvua.
“TANROADS waelimisheni wananchi ili wazuie wenzao kulima, kujenga na kuchunga mifugo kwenye hifadhi za barabara ili kulinda barabara na kuzikarabati kwa urahisi inapohitajika”, ameelekeza Kasekenya.
Amessma, Mkoa wa Pwani ni mkoa wa Viwanda hivyo ujenzi na ukarabati wa barabara hizi za Kilwa na Mkuranga-Kisiju KM 45 uzingatie ubora na viwango vya juu ili kuwezesha magari makubwa kusafirisha malighafi na bidhaa za viwandani kwa urahisi wakati wote.
“Kukamilika kwa barabara ya Mkuranga -Kisiju kutaongeza tija kwenye bandari ya kisiju na hivyo kuvutia wawekezaji wa Viwanda na Hotel”, amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.
Naibu Waziri Kasekenya amesema Serikali iko katika hatua za mwisho kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kufanya ukarabati mkubwa kwenye maeneo yote ya barabara na madaraja yalioathiriwa pakubwa na mvua zilizonyesha mwaka huu.
Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani, Eng. Zilli Kihoko amesema watahakikisha hifadhi za barabara, maeneo ya maegesho na madaraja yanalindwa ili yadumu na kuleta tija kwa wananchi.