Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ametembelea Shule ya mpya Wasichana ya (Manyara Girls), na kuongea na Wanafunzi pamoja na kuwakaribisha rasmi Mkoani Manyara wanafunzi 110 waliowasili shuleni hapo na kuanza masomo yao ya kidato cha tano kwa mchepuo wa Sayansi (PCM na PCB).
Sendiga ameenda shuleni hapo akiwa amevalia Sare sawa na wanafunzi wa shule hiyo jambo ambalo limewashangaza na kufurahisha wanafunzi pamoja na Walimu ambapo ameagiza umaliziaji wa miundombinu yote ambayo bado haijakamilika ikamilike mapema, ili wanafunzi waweze kupata huduma hizo hasa ya Bwalo.
Aidha, amewashukuru na kuwapongeza wazazi walioleta watoto wao katika shule hiyo mpya na kuwahakikishia watoto wao watapata Elimu na huduma bora, ulinzi na usalama wakati wote watakapo kuwepo shuleni hapo.