Wakili Msomi na Mwanadiplomasia mzoefu Chikulupi Njelu Kasaka, amachukua fomu ya kuwania nafasi ya ubunge wa Afrika Mashariki (EALA) iliyotangazwa na Katibu wa bunge, ya kujaza nafasi ya wazi ya kundi la wanawake kupitia chama cha Mapinduzi (CCM)
Wakili Chikulupi amesema, miongoni mwa vipaumbele vyake kama atachatachaguliwa na wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mwakilishi wao, atahakikisha nchi zinafanya biashara bila vikwazo.
Wakili Chikulupi ameyasema hayo leo Jumatano Agosti 14, 2024 baada ya kuchukua fomu za kugombea Ubunge wa Jumuiya hiyo katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma.
Chikulupi Njelu Kasaka kitaaluma ni Mwanasheria na Wakili, ni mbobezi wa masuala ya siasa, utawala na diplomasia mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 12 katika mahusiano ya kimataifa na diplomasia.
Wakili Chikulupi amekitumikia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika nyanja tofauti na pia ni mjumbe katika kamati mbalimbali.
Uchaguzi wa Mwakilishi wa Bunge la Afrika Mashariki unakuja baada ya siku chache mwakilishi wa jumuiya hiyo kufariki dunia Juni, 2024.