Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuhudhuria Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utafakaonyika Agosti 17, 2024 jijini Harare, Zimbabwe.

Rais Dkt. Samia anatarajia kuondoka nchini hii Agosti 15, 2024 kuhudhuria Mkutano huo wenye kauli mbinu: “Kukuza ubunifu ili kufungua fursa za ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu kuelekea SADC yenye viwanda.”

Katika Mkutano huo, Rais Dkt. Samia anatarajia kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC akipokea kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Hakainde Hichilema anayemaliza muda wake.

Tetesi za usajili Duniani leo Agosti 15
Madrid yaandika historia Mbappe akiipa kombe la UEFA