Klabu ya Real Madrid imefanikiwa kushinda ubingwa wa UEFA Super Cup baada ya kuifunga Atlanta mabao 2-0.Madrid walipata bao la kwanza dakika ya 58 kupitia kwa Valvede aliyemalizia pasi kutoka kwa Vincious Junior na bao la pili liliwekwa kimiani dakika ya 69 na  mshambuliaji mpya Kylian Mbappe.

Ubingwa huo unaifanya Real Madrid kufikisha makombe 6 na ndiyo timu yenye makombe mengi zaidi tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo mwaka 1974. Kocha Carlo Anceloti amefikisha makombe matano ya michuano hiyo alitwaa makombe mawili akiwa na AC Milan na makombe matatu akiwa na Real Madrid.

Tathmini ya mchezo 

Kocha Ancelloti hakuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchezaji na machaguo ya wachezaji katika mchezo huo. Eneo la ulinzi liliongozwa na Tibout ,militao,carvajal,Mendy na Rudiger. Eneo la kiungo liliundwa na Tchouameni,Bellingham na valverde huku eneo la ushambuliaji liliundwa na Mbappe ,Vinicious jr na Rodrigo akitumia mfumo wa 4-3-3.

Real Madrid waliutawala mchezo huo na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.Kila mchezaji aliyeanza kwenye mchezo huo alionyesha uwezo mkubwa na hii ikazidi kuonyesha klabu hiyo iko imara sana na tutegemee ikifanya vizuri kwenye michuano mbalimbali itakayooshiriki likiwemo kombe la dunia la vilabu,UEFA ,La Liga na michuano ya Copa De Ray

Ushindi huu unamaana gani kwa Mbappe

Huu ni mchezo wa kukumbukwa zaidi kwa Mbappe kwani hakuwahi kutwaa Kombe la UEFA akiwa na PSG wala Monaco AS. kutwaa Kombe hilo kirahisi zaidi tena katika mchezo wake wa Kwanza akiwa na Real Madrid kunamwongezea ujasiri wa kuamini yupo sehemu sahihi na ni wakati wake wa kuonyesha ukubwa wake duniani.

 

 

Rais Samia kuondoka Nchini leo
RCT watabasamu bei mpya ya Mchele kwa Wakulima