Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Juma Khatib, amesema wameridhishwa na utekelezaji wa falsafa ya 4R, inayotumiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Khatib ameyasema hayo hii leo Agosti 15, 2024 kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma. katika Mkutano wa kutoa Tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27, 2024.

Amesema, tangu Rais Samia ameingia madarakani, mazingira ya Vyama vya Siasa kufanya shughuli zake yamekuwa rafiki kwa vyama ikiwemo kuondoa zuio la Mikutano ya hadhara.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utahusisha Wenyeviti wa Vijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Vijiji, Wenyeviti wa Mitaa, Wajumbe wa Kamati za Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji.

TCB kushirikiana na Bunge kuwainua Wajasiriamali
Mchengerwa afafanua taratibu uchaguzi Serikali za Mitaa