Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema hadi kufikia Septemba Mosi 1, 2024 jengo jipya la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kisongo litaanza kutumika.

Makonda ameyasema hayo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja huo Jijini Arusha hii leo Agosti 16, 2024 wenye uwezo wa kuhudumia Watu 1000 kwa pamoja.

Amesema, “tumetembelea Kisongo Airport kuondoa maendeleo ya ujenzi, kazi inaendelea na inatupa faraja na tuliongea na DG tunataka uwanja huu ufanye kazi usiku na mchana na pia ukatumika kwa wenye private jet.”

Makonda ameongeza kuwa, “taarifa tulizopata kutoka kwa Injinia wetu Wasimamizi wa mradi ni kwamba September 1,2024 jengo letu hili litaanza kufanya kazi ambalo linatoka hatua ya kubeba Watu 150 kwenye jengo la zamani kwenda kuwabeba Watu 1000 kwa wakati mmoja.”

Katika hatua nyingine, Makonda ameagiza kutumika kwa teknolojia katika utoaji wa huduma kwa abiria wanaotumia uwanja huo pamoja na kuweka miundombinu ya kutangaza utalii wa Arusha, ili kuvutia zaidi watalii.

Familia yamuangukia Rais Samia usaidizi ardhi iliyoporwa
Miswada ya Sheria: Kamati yaanza kupokea maoni ya wadau