Umoja wa Mataifa – UN, umeomba siku saba za kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza, ili kutoa nafasi kwa zaidi ya watoto 640,000 kupewa chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio.
UN imeyasema hayo mapema wiki hii, ambapo imedai kuwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanataka kutoa chanjo hiyo ya matone, kwa watoto wenye umri chini ya miaka 10.
Aidha, imebainisha kuwa bila kuwepo kwa usitishwaji wa muda wa mapigano hayo kwa ajili ya kutoa huduma za kiutu, ufikishwaji wa chanjo hizo hautafanikiwa.