Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Tamasha la Kizimkazi ni fursa muhimu kwa Mkoa wa Kusini kuongeza vivutio vya utalii na kuwavutia wawekezaji kuwekeza katika mkoa huo.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo hii leo, Agosti 18 2024, katika Ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi, lililofanyika Kizimkazi Dimbani, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kumaliza changamoto zinazoukabili Mkoa wa Kusini ikiwa ni pamoja na uhaba wa wafanyakazi sekta ya afya kabla ya kufikia mwaka 2025.

Dkt. Mwinyi amefafanua kuwa, mbali na kuimarisha utalii wa ndani, tamasha hilo linaleta umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi pamoja na kuimarika kwa mila, desturi, na maadili ya Kizanzibari.

Tamasha hilo litaendelea kwa matukio mbalimbali hadi Agosti 25, 2024 ambapo litafungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Tiba Radiolojia: Wajadili mbinu kuongeza wigo wa huduma
Mavunde asikiliza changamoto za Wachimbaji wadogo Simanjiro