Wawakilishi wa mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney wako kwenye mazungumzo na klabu ya Saudi Pro League Al-Ahli ili kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Teamtalks).Manchester United hawana nia ya kutaka kumnunua Toney. (Sky Germany).

Manchester City wanataka meneja Pep Guardiola, 53, kuamua iwapo atasaini mkataba mpya na klabu hiyo kabla ya Krismasi. Mkataba wa sasa wa Mhispania huyo utaendelea hadi 2025. (Sky Sports)

Nottingham Forest, Villarreal, Sevilla, na Valencia wanataka kumnunua beki wa Aston Villa na Uhispania Alex Moreno, 31. (Football Insider).

Panathinaikos iko kwenye mazungumzo na Manchester United kuhusu mkataba wa kiungo wa kati wa Uruguay Facundo Pellistri, 22. (Athletic – Subscription Required).

Atletico Madrid hawajapuuza uhamisho wa kiungo wa kati wa Valencia na Uhispania Javi Guerra mwenye umri wa miaka 21 huku mkataba wao wa kiungo wa kati wa Chelsea na Muingereza Conor Gallagher, 24, ukikwama. (Subscription Required)

Liverpool itasubiri hadi dirisha la usajili la Januari kumsajili kiungo nyota baada ya hatua ya klabu hiyo kumnunua Mhispania Martin Zubimendi, 25, kutoka Real Sociedad kushindikana. (Football Insider).

Fulham wameanzisha tena mazungumzo na Manchester United kuhusu usajili wa kiungo wa kati wa Scotland Scott McTominay, 27. (Sky Sports).

.

Mkurugenzi wa michezo wa Napoli Giovanni Manna amekataa kufuta mpango wa kumnunua McTominay. (Manchester Evening News)

Klabu hiyo ya Serie A pia imekubali mkataba wa kumsajili winga wa Brazil David Neres, 27 kutoka Benfica. (Fabrizio Romano).

Las Palmas wamewasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Fulham raia wa Brazil Carlos Vinicius, 29, ambaye pia anasakwa na Corinthians. (Sky Sports).

Crystal Palace wamefanikiwa katika kumsaka beki Mfaransa Maxence Lacroix, 24, kutoka Wolfsburg. (Sky Germany).

Maisha: Hizi hapa mbinu za kupanda cheo kazini
Watakiwa kuyaishi kwa vitendo Mafunzo utekelezaji shule salama