Takribani Watu 13 wamefariki hii leo Agosti 20, 2024 majira ya asubuhi baada ya magari kadhaa, ikiwemo basi lililobeba abiria 60, kuhusika katika ajali mbaya eneo la Salgaa kwenye barabara kuu ya Nakuru-Nairobi nchini Kenya.

Taarifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu imeeleza kuwa katika ajali hiyo, watu 36 wamejeruhiwa ambapo Maafisa wa Polisi lwalifuka eneo la tukio kutoa usaidizi wa uokozi wa manusura waliokuwa wamekwama kwenye mabaki ya magari husika.

“Watu 36 waliojeruhiwa wamepelekwa katika Hospitali za Molo na Coptic kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha basi la abiria na magari mengi eneo la Migaa huko Molo, Kaunti ya Nakuru,” imeeleza taarifa hiyo.

Basi hilo lilikuwa likielekea Mombasa kutoka mjini Kakamega na lilipopoteza uelekeo kisha kugonga gari ndogo iliyosababisha kuyaparamia magari mngine kabla kuanguka pembezoni mwa barabara.

 

Wakati huo huo, polisi wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo na licha ya juhudi kubwa za uokoaji, kuna hofu kwamba watu zaidi wanaweza kuwa bado wamenaswa ndani ya mabaki ya basi hilo la abiria na hali yao haijulikani.

Maisha: Umekuwa ukipoteza pesa? Soma hapa
Urembo: 'Makeup' kwenye Vita ya kwanza ya Dunia