Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, kimelaani kukamatwa na kuendelea kushikiliwa kwa Viongozi wake wa Wilaya ya Temeke wakidai kitendo hiko ni kinyume cha sheria.
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje John Mrema, kupitia taarifa yake amewataja Viongozi hao kuwa ni Katibu wa Jimbo la Temeke, Jacob Mlay na Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Temeke, Deusdedith Soka.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, “Tunalitaka Jeshi la Polisi liwaachie mara moja bila masharti na kama wametenda kosa lolote wafikishwe Mahakamani mara moja, aidha Polisi ieleze inakowashikilia ili waweze kupatiwa msaada wa kisheria na mahitaji muhimu ya kibinaadamu.”