Phil Foden amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa nchini Uingereza (PFA).Foden alikuwa akiwania tuzo hiyo pamoja na wachezaji wenzake wa Manchester City ambao ni Halaand na Rodri. Tuzo hii inakuwa ya nne kwa Manchester City ndani ya miaka mitano chini ya kocha Pep Guardiola. Kelvin De Bruyne ametwaa tuzo hiyo mara mbili mfululizo msimu wa 2019/20 na 202o na 21. Halaand alitwaa tuzo hiyo msimu wa 2022/23 na Foden ametwaa tuzo hiyo msimu wa 2023/24.
NINI KIMEMPA TUZO HIYO PHIL FODEN
Wachezaji wa Manchester City walimchagua Foden kama mchezaji bora wa timu hiyo kwa msimu wa 2023/24 baada ya kufunga mabao 27 na kuchangia mabao 12 akiisaidia timu hiyo kutwaa makombe ya Ligi kuu Uingereza, Kombe la Dunia la vilabu,UEFA SUPER CUP, Robo fainali ya UEFA,Ngao ya jamii na kucheza fainali za FA. Mchezaji huyo aliingia kinyang’anyilo cha uchezaji bora wa msimu na Halaand,Rodri,Cole Palmer ,Martin Oodergard na Watkins.Mshindani wake wa karibu alikuwa ni Cole Palmer kutoka Chelsea aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi.
MWANZO MZURI KWA FODEN?
Mpaka sasa Foden ameshinda makombe 18 akiwa na Manchester City,mchezaji huyo amewahi kutwaa tuzo za mchezaji bora chipukizi mara mbili kwa misimu ya 2020/21 na msimu wa 2021/22. Mbali na tuzo za PFA mchezaji huyo alitwaa tuzo ya chama cha waandishi wa habari za michezo Uingereza .Tuzo hizi zinamfanya mchezaji huyo kutwaa kila tuzo inayotolewa ndani ya Uingereza.
Foden mwenye miaka 24 anatajwa kama mchezaji mwenye uwezo mkubwa na msimu wa 2024/25 anategemewa kufanya makubwa ikiwamo kutetea kombe la ligi kuu Uingereza lakini kuonyesha uwezo mkubwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ili msimu ujao aweze kuingia kwenye kinyang’anyilo cha mchezaji bora wa dunia.
Foden ametajwa kwenye kikosi cha wachezaji bora wa msimu akiwa sambamba na Halaand, Rodri na Kelvin De Bruyne wachezaji wenzake kutoka Manchester City.