Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa watanzania kuwekeza katika elimu kwa watoto ikiwemo elimu ya dini kwa lengo la kukabiliana na mmomonyoko wa maadili unaolikabili Taifa.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Chemba akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi mkoani Dodoma.

Amesema, ili Taifa liweze kupiga hatua za haraka linahitaji wananchi waliopata elimu. Amesema kila mzazi na mlezi ni wajibu kusimamia na kuhakikisha watoto wanajengwa katika maadili mema kwa kupata mafundisho mazuri ya dini na kusisitiza umuhimu wa kutunza mazingira ikiwemo kukomesha ukataji miti ovyo, kuacha kuchoma moto wakati wa kuandaa mashamba ya kilimo pamoja na uharibifu wa vyanzo vya maji.

Amesema athari ni kubwa zinazotokana na uharibifu wa mazingira ikiwemo kuanza kupata magonjwa, vifo vya Wanyama na binadamu, ongezeko la joto na ukosefu wa maji, huku akiwahimiza viongozi kusimamia zoezi la upandaji miti hususani wakati mvua zitakapoanza na kusimamia miti hiyo kuhakikisha inafikia lengo.

Makamu wa Rais pia amesema Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya watanzania kutumia nishati safi ya kupikia na kudai kuwa Serikali imedhamiria kuanzisha mfuko maalum ili kuweza kutoa ruzuku na kuwawezesha wananchi wa kawaida kutumia majiko ya gesi.

default

Amezihimiza Taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 kwa siku kuanza kutumia nishati safi ya kupikia kwa kuachana na ukataji miti kwaajili ya kuni na mkaa wa kupikia na kuwasihi wananchi wa Wilaya ya Chemba kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuzingatia kutunza amani iliyopo nchini.

Awali, Makamu wa Rais akiwa wilayani Chemba amezindua Mradi wa Jengo la Ofisi ya Halmshauri ya Wilaya Chemba ambao umegharimu shilingi Bilioni 4.6.

Kwa mwenendo huu Arteta anastahili kubaki Arsenal?
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Agosti 22, 2024